1 Corinthians 1:5-10

5 aKwa kuwa katika Al-Masihi mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, 6 bkwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Al-Masihi ulithibitishwa ndani yenu. 7 cKwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi. 8 dAtawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. 9 eMungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Isa Al-Masihi, Bwana wetu ni mwaminifu.

Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa

10 fNawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi.
Copyright information for SwhKC